Mambo Matano ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Kitu Mtandaoni
Kutokana
na ukubwa wa teknolojia sasa watu wengi wameanza kufanya biashara
mtandaoni, kuchangia hapo watu wengi nao pia wameanza kununua bidhaa
mbalimbali mtandaoni iwe ni kwenye instagram, facebook au hata kwenye
tovuti mbalimbali biashara mtandaoni kwa sasa imekua kubwa sana, lakini
ulishawahi kujiuliza ni mambo gani ya kuzingatia kabla ujanunua kitu
chochote kwenye mitandao hiyo.? Yafuatayo ni mambo hayo.
- Nununa Kitu Kutoka Mahali Panapo Fahamika (Maarufu)
Kumbuka
kuwa makini sana wakati unataka kununua kitu kwenye mtandao tena hasa
kwa watu ambao siyo rasmi, kwa mfano kununua kitu mahali ambapo
hapajulikani ni kitu cha hatari sana uwezekano wa kutapeliwa au kupata
bidhaa isiyo staili ni mkubwa sana. Hivyo ni vyema kununua mahali ambapo
unajua angalau watu kadhaa ambao wamesha wahi kununua hapo, pia kama
ukifanikiwa kujua mahali ofisi ilipo itakuwa ni vizuri zaidi na
itakusadia pale unapotaka kurudisha kitu.
- Nunua Kitu Kutoka Mahali Ambapo Panatoa Warranty (udhamini)
Mfanya
biashara yoyote ambae anajiamini hato ona shida kukupa warranty ya
bidhaa unayo nunua hivyo ni vyema wakati unataka kununua kitu kwenye
mtandao kuuliza warranty kwani hiyo ni njia moja wapo ambayo
itakuonyesha bidhaa hiyo ni bora sambamba na huduma inayotolewa na mtu
au kampuni inayokuuzia kitu mtandaoni. Kumbuka kuna baadhi ya vitu
havina warranty ila kama hakifahi au sio sawa na ulicho agiza ni muhimu
kupewa nafasi ya kurudisha na kuchukua kingine hivyo ni vyema kuuliza
hayo kabla ya kununua.
- Nunua Mahali Ambapo Wanatoa Risti
Risiti
ni muhimu sana sio kwa serikali pekee bali hata kwako wewe tena hasa
unaponunua kitu cha bei ghali, risiti ndio kielelezo kinacho onyesha
kuwa kweli umenunua bidhaa kutoka kwa kampuni au mtu huyo, mafanya
biashara yoyote anae uza bidhaa mtandaoni bila risiti ni vyema kuwa
makini nae kwani kwa kununua bidhaa kwake kutakuwa hakuna namna ya kujua
kama mliuziana bidhaa yoyote hasa pale inapotokea tatizo lolote.
- Fanya Uchuguzi wa Bidhaa Unayotaka Kununua Kabla ya Kununua
Hili
ni muhimu sana tena kama ndio mara yako ya kwanza kununua bidhaa
mtandaoni ni vyema kujua vizuri bidhaa hiyo ili pale unapoletewa bidhaa
hiyo uweze kuitambua kwa urahisi na kwa haraka zaidi kuliko kubambikwa
kitu ambacho baadae ndio unajua kuwa sio kitu sahihi au bidhaa hiyo
haikukamilika. Hivyo fanya ukuchunguzi kwa kamilika ikiwa ni pamoja na
kuulizia kuhusu bidhaa hiyo kutoka kwa mtu au kampuni unayotaka kununua.
- Nunua Bidhaa Siku Moja Baada ya Kuamua Kununua
Hili
pia ni muhimu kwani pale unapotaka kununua bidhaa mtandaoni ni vyema
kupata nafasi ya kufanya uchaguzi wako kwa umakini ikiwa ni pamoja na
kuangalia sehemu unayotaka kununua bidhaa yako ni vyema kulizia kuhusu
sehemu unayotaka kununua ikiwezekana nenda kwenye ofisi kabla ya
kununua, hii itakupa uwezo wa kujua vizuri sehemu unayotaka kununua
bidhaa yako pamoja na bidhaa unayotaka kununua kama uko mbali na ofisi
basi fanya uchunguzi wa mtandao huo au page hiyo kwa kuangalia bidhaa
mbalimbali pamoja na maoni ya watu mbalimbali.
Na hayo ndio baadhi
tu ya mambo ambayo ni muhimu kuzingatia kabla ya kununua bidhaa yoyote
mtandaoni, unaweza kuongeza baadhi ya mambo kwa kutuandikia kwenye maoni
hapo chini nasi tuta yaongeza kwenye makala hii.
USISAHAU KUMSHIRIKISHA MWENZAKO KUHUSU UKURASA HUU
0 comments:
Post a Comment