LG Yazindua Kioo Kikubwa cha Kompyuta cha Inch 42.5
Kampuni
ya LG sasa imetangaza kuja na kioo kikubwa cha inch 42.5 kwaajili ya
kompyuta, kioo hicho ambacho kinauwezo wa kuenea vioo vinne vya kawaida
kinakuja na teknolojia ya UHD huku ikiwa na resolution ya 3840×2160 kwa
maana nyingine kioo hichi kinauwezo wa teknolojia mpya ya 4K.
Mzigo huu kutoka LG unakuja na sehemu au port nne za kuchomeka waya (cable) za HDMI pamoja na sehemu mbili za kuchomeka USB zikiwa na uwezo wa USB 3.0 zote zikiwa zime tengenezwa kwa teknolojia ya KVM switch, haija ishia hapo kuongezea kwenye kioo hicho sasa kuna sehemu ya USB Type-C yenye teknolojia ya DP Alt Mode pamoja na spika mbili za harmon/kardon speakers zenye uwezo wa 10W huku ikiwa na sehemu ya headphone jack kwaajili ya kuchomeka spika au hadphone za nje.
Kioo hicho chenye jina la 43UD79-B kinakuja pia na remote ambayo unaweza kutumia kwa matumizi mbalimbali kama vile kufanya full screen, kuzima na kuwasha, kuongeza mwanga, kuongeza sauti, kurekebisha aina ya picha na mengine mengi.
Kioo
hichi kinategemea kutoka mwezi May 19th, 2017 kwa nchini japan na
inategemewa kuuzwa kwa dollar za kimarekani $745 USD sawa na shilingi za
kitanzania Tsh 1,700,000. Itakubidi usubiri mpaka mwezi wa sita au wa
saba mpaka kuipata hii kwa hapa Tanzania.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea MJUZI ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka.
Mzigo huu kutoka LG unakuja na sehemu au port nne za kuchomeka waya (cable) za HDMI pamoja na sehemu mbili za kuchomeka USB zikiwa na uwezo wa USB 3.0 zote zikiwa zime tengenezwa kwa teknolojia ya KVM switch, haija ishia hapo kuongezea kwenye kioo hicho sasa kuna sehemu ya USB Type-C yenye teknolojia ya DP Alt Mode pamoja na spika mbili za harmon/kardon speakers zenye uwezo wa 10W huku ikiwa na sehemu ya headphone jack kwaajili ya kuchomeka spika au hadphone za nje.
Kioo hicho chenye jina la 43UD79-B kinakuja pia na remote ambayo unaweza kutumia kwa matumizi mbalimbali kama vile kufanya full screen, kuzima na kuwasha, kuongeza mwanga, kuongeza sauti, kurekebisha aina ya picha na mengine mengi.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea MJUZI ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka.
0 comments:
Post a Comment