Ukiangalia historia ya vitabu vitakatifu kama biblia, kabla
ya gharika ya nuhu watu walikua hawaruhusiwi kula nyama kabisa, ila waliruhusiwa kula matunda na mboga mboga
za kondeni. Sidhani kama mungu aliwakataza kwa bahati mbaya kwani miaka ya sasa
tafiti nyingi zinaonyesha watu wanaokula nyama wanapata magonjwa mengi kuliko wale wasio kula
na pia atu wasiokula nyama huishi muda mfupi kuliko wasiokula na hata kwenye
historia ya biblia inaonekana watu wa zamani waliishi miaka mingi sana
ukilinganisha na walioishi baada ya gharika yaani sisi.
Lakini hata hivyo historia inaonyesha kwamba hata kabla ya
gharika la nuhu watu waliasi na kuanza kula nyama na baadae baada ya gharika
mungu aliamua kuruhusu kuliwa kwa baadhi
ya nyama na kukataza baadhi ya nyama. Siku moja nilikua naongea na mchungaji
mmoja msabato kuhusu sheria zao za kula nyama na vyakula mbalimbali nikagundua
kwamba sio sababu za kibiblia tu kwani kuna vitu wasabato hawatumii vitu kama
majani ya chai, soda za cocacola na kadhalika lakini kwa sababu za kiafya
zaidi. Leo tutangalia madhara ya kula nyama… lakini kabla ya
kuangalia madhara ya nyama kuna makundi makuu mawili ya nyama yaani nyama nyekundu na nyama nyeupe.Nyama nyekundu ni
ile ambayo ina rangi nyekundu kabla ya kupikwa mfano nguruwe, ng’ombe,mbuzi, na
wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne.Nyama nyeupe ni zile ambazo zina rangi
nyeupe kabla ya kupikwa mfano kuku, bata, samaki, mbuni na wanyama wote
wanaotembea kwa miguu miwili.
Utafiti unaonyesha ulaji wa nyama nyekundu una
madhara makubwa sana kuliko ulaji wa nyama nyeupe hata hivyo watu ambao hawali
nyama kabisa wako mbali sana na hatari hizi. Lakini kwa kua nyama pia ina faida
katika miili yetu basi nyama nyeupe ni salama sana kuliko nyekundu.Hebu tuangalie
madhara ya nyama kama ifuatavyo.
Hatari ya kupata magonjwa ya moyo: nyama ina kitu kinaitwa
lehemu kitaalamu kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu
na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri..hii husababisha viuongo muhimu vya
mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol
ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii
inayoongezeka kutoka kwnye nyama ni hatari sana.[nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi]
Kansa ya utumbo mkubwa; nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa
ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti
unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa
kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara ya haya yameonekana kutokuwepo kwa kula
nyama nyeupe.
Ugonjwa wa kisukari; utafiti mpya umeonyesha kwamba watu
wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi
mfulululizo[cohort studies}… watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa
kisukari sana kuliko wale wasiokula.
Hatari ya kupata ugonjwa wa alzheirs disease; huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu
wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza kumbukumbu kabisa. Wanasayansi wanaamini
protini inayopatikana kwenye nyama kwa jina la Tau and beta-amyloid huharibu
mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia kwa ugonjwa huu.
Ugonjwa wa kifafa; minyoo inyopatikana kwenye nguruwe
kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya
fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa
nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.
Unene uliopitiliza; nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha
mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya
nguruwe.unene na kitambi ni hatari sana
kwana husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla
vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.
Nyama tunazokula siku hizi sio nyama halisi tena;
ukiangaliwa nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na hotel kubwa
hapa Tanzania hapa namaanisha kuku sa kisasa, zinakuzwa kwa kemikali nyingi
sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti
kabisa na kuku wa kienyeji. Lakini kwasababu wamiliki wa biashara za nyama ni
watu wenye fedha nyingi sana duniani ukweli huu hufichwa.
Magonjwa ya wanyama husika; miaka ya sasa dunia imekua
inakumbwa sana na magonjwa ambayo yanashambulia wanyama. Yameua watu wengi na
mengine hayatibiki kabisa. mfano mafua ya ndege, ugonjwa wa ukimwi ambao historia
inasema ulitoka kwa kula nyama ya nyani wa porini, na ugonjwa wa ebola ambao
virusi vyake huishi kwenye nyama wa popo.
Mwisho; nyama ya nyeupe yaani samaki, kuku, bata na ndege
wengine wanaoruhusiwa kuliwa ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama mbuzi,
ng’ombe, nguruwe na wengine ni hatari sana. Na kama wewe tayari una tazizo la
moyo, presha, kisukari na kansa huu ni wakati sahihi wa kuacha kula nyama
nyekundu kabisa kwani hizo nyama zitakupeleka kaburini.ENDELEA KUFATILIA MAKALA ZA MJUZI NIKUJUZE ZAIDI.
Nitaaanza kuchunga kutokula nyamA
ReplyDeletekaribu
ReplyDelete