Ujenzi wa nyumba ya kuishi ni jukumu ambalo kila mtu hulifikiria pale anapofikisha umri fulani wa kujitambua, mara nyingi sio kila mtu anayefikiria hupata fursa ya utekelezaji la hasha hutegemea kipato cha mtu na bajeti yake na ndiyo maana nyumba hutofautiana pia katika ubunifu na malighafi(material) zitakazo tumika.
Kwa ufupi katika ujenzi wa nyumba ya kuishi kuna hatua nne za kuzingatia;
1. Msingi – hii ni hatua ya kwanza ya ujenzi wa nyumba baada ya kumaliza uchoraji wa ramani na upimaji wa kiwanja na nyumba itakavyokaa (setting out)
2. Upandishaji wa ukuta – hii ni hatua inayofuata baada ya msingi. angalia picha hapo chini
3. Uwezekaji
4. umaliziaji – hii ndiyo hatua ya mwisho na ndiyo hatua ambayo mtu anaweza kuhamia. hatua hii inavitu vingi sana hivyo basi ili uweze kuhamia itakubidi uhakikishe vitu vifuatavyo vya hatua hii umevikamilisha, madirisha, milango(sana sana ya kutokea nje), uwekaji wa mabomba kwa ajili ya umeme na maji, kusakafia(flooring) na kupiga lipu (plaster)
Kumbuka: Lengo la kukuwekea mada hii ni kukupa a,b,c.. wewe unayefikiria kujenga au umeshajenga sasa unataka kuhamia. Bonyeza maandishi ya blue hapo chini kwa mahitaji ya ramani za majengo.
HILI NDIO SULUISHO LA RAMANI
0 comments:
Post a Comment